Katika umri huu, watoto wanajua kuwa unaweza kuwa mgonjwa kutokana na mabadiliko ndani na si tu kwa sababu ya nguvu za nje. Magonjwa sasa hayaonekani kama muujiza wala adhabu, lakini yanaweza kusababishwa na maambukizi ya bakteria au virusi. Hata hivyo, kufikiria kimuujiza kunaweza kutokea hadi miaka ya ujana wakati wa msongo wa mawazo. Wanaufahamu mwili wao vizuri zaidi kuliko awali. Wanaweza kuona tiba kama inayodhuru au kuhofia kuwa mwili utabadilishwa. Kama tu watoto wachanga wanavyosema sehemu ya mwili wao itakayotibiwa na sehemu ambazo hazitatibiwa.
Watoto wa umri huu wanaweza kuhofia vifaa wanavyoona katika chumba cha upasuaji. Pia ni katika umri huu ambapo wanaanza kufikiria kuhusu kifo. Wanaweza kuhusisha kulala na kifo na watoto wengi wachanga wanahofia kuwa hawataamka baada ya upasuaji. Wahakikishie kwa kusema kuwa watatunzwa kwa makini wakati wote wanapolala na hadi wanapoamka kabisa.
Anza kumwandaa mtoto katika rika hili wiki moja kabla ya kuenda hospitalini. Watoto katika rika hili huonyesha mvuto mkubwa wa kile kitakachotendeka wakilinganishwa na watoto wachanga. Kwa hivyo, kuwaandaa kunapaswa kulingana na maswali wanayouliza. Wahimize kutumia mchoro kukuambia kuhusu mawazo na hofu zao.