Watoto na vijana wanaweza kukumbwa na hofu na msongo wa mawazo kuhusu ziara za huduma ya afya na upasuaji Huenda wakahitajika kuingia katika mazingira mapya na wasiyoyazoea, kukutana na watu wapya na kukabiliana na desturi mpya. Huenda wakachunguzwa, kutoa sampuli za vipimo, kutibiwa na labda kufanyiwa upasuaji kwa kutumia nusukaputi. Matukio na hali kama hizo mara nyingi hukumbukwa mambo yote yawe mazuri, au hata matatizo yakitokea au tiba ikikumbwa na utata. Hii inaweza kuwa na madhara ya muda mfupi na muda mrefu kwa watoto, vijana na familia, kwa hivyo kila jitihada zinafanywa kupunguza athari hizi.
Maandalizi yanayofaa hupunguza msongo wa afya na wasiwasi kwa watoto na vijana. Hii inarahisisha upasuaji na kupunguza athari yoyote hasi ya muda mfupi au muda mrefu. Husaidia kukabiliana na kilichotendeka na kuvumilia vizuri kwa huduma ya afya na matibabu siku zijazo. Ili kuweza kuchakata na kuelewa wanachosikia, kusoma, kuona na kushuhudia, pia ni muhimu kwa watoto na vijana kupewa nafasi za mara kwa mara ili kujiandaa wenyewe kwa njia tofauti.
Kama mzazi au mlezi, unamjua mtoto wako vyema. Wewe ni kiungo muhimu zaidi kati ya mtoto wako na sisi tunaofanya kazi hospitalini Unatoa msaada muhimu sana kwa mtoto wako. Ni muhimu kuwa uhisi una habari za kutosha na salama kuhusu hali. Kwa hivyo, turuhusu tukusaidie kujiandaa na kuelewa vyema.
Tafadhali pia tufahamishe ikiwa wewe au mtoto wako mna wasiwasi zaidi kuhusu kile kitakachotendeka, au ikiwa mna masuala mengine yoyote. Tupo hapa ili kuyajibu maswali yako na kukusaidia.