Vijana

Miaka ya ujana ni wakati wa mabadiliko makubwa ya kimwili na hisia katika maisha ya mtu.Kuhofia kuhusu kutokuwa kawaida au sawa kabisa ni jambo la kawaida.

Vijana wanafikiria kila kitu kinawahusu. Mara nyingi wanafikiria kuwa hakuna mtu mwingine amewahi kupitia mambo kama hayo au alikuwa na hisia sawa kama wao. Kukubali usaidizi wa utendakazi wa mwili kutokana na ugonjwa ni jambo gumu kwa kijana kukabiliana nalo, kwa kuwa hili linamfanya kuhisi kutokamilika na kudhibiti mambo.

Miaka ya ujana ni wakati wa ukombozi na haja ya kujiamulia mambo. Vijana wana haja kubwa ya kurudi nyuma na kuonyesha dhahiri hadhi yao kwa kujitenga na familia yao ya karibu. Ongezeko la kutegemea, linaloweza kuwa madhara ya asili ya ugonjwa, linaweza kuwa suala gumu kwa kila anayehusika. Hata hivyo, mtu anayeonyesha ujasiri, mara nyingi unapata mtu mdogo mwenye wasiwasi ambaye anahitaji usaidizi mkubwa na kwenye moyo wake mkubwa, anashukuru sana kwa usaidizi

Kuhusiana na nusukaputi, mara nyingi kuna hofu ya kuamka katikati ya shughuli ya upasuaji au kutoamka kabisa baadaye. Pia kuna wasiwasi kuhusu kukosa kujidhibiti, kusema kitu kisichofaa au kutoweza kudhibiti kibofu chake au matumbo yake.

Vijana wanataka kutiliwa maanani, kuheshimiwa na kuandaliwa kama watu wazima. Kwa jumla wana maarifa ya kutosha ya kibayolojia kuelewa jinsi mwili na mfumo wa ogani unavyofanya kazi. Wanaweza kufikiria kinadharia, kufanya maamuzi kutoka kwenye taarifa waliyopewa na kutambua madhara ya hatua zilizowekwa. Kwa hivyo vijana hawaridhiki kwa kuambiwa tu kitakachotendeka wakati wa upasuaji au matibabu fulani. Wanataka taarifa pana kuhusu kipindi kizima cha huduma, uchunguzi na matibabu yanayofanywa na athari zinazotarajiwa. Vijana wanapaswa kuhimizwa kuuliza maswali na kujumuishwa katika majadiliano, vipindi vya maswali na majibu na maamuzi yanayowahusu. Kuwaandaa kunapaswa kuanza wakati unaofaa ili kuwapa nafasi ya kutafakari na kuwaza.