Mikabiliano ya watoto na vijana kwa kukaa hospitalini, nusukaputi na upasuaji

Mikabliano ya watoto na vijana hutegemea umri, uelewa, utambuzi wa ugonjwa, tiba na hali zao za kutumia huduma ya afya.

Baadhi ya watoto huonekana kukabiliana na hali za kukaa hospitalini bila hata kutambua, ilhali wengine huathirika zaidi, wengine moja kwa moja, wengine baadaye. Mikabiliano hii inaweza kuwa migumu kuelewa na inaweza kutokea nyakati fulani au kutohusiana na huduma ya matibabu. Mikabiliano inaweza kuonekana kama ya kuwa na wasiwasi; kutamauka, kujitenga, au kutozungumza; kutoshughulika; au matatizo ya kusikia au kulala. Unapaswa kuangalia mikabiliano hii na kuhakikisha kuwa uko tayari kumsaidia mtoto wako ikitokea. Watoto na vijana wengi wana ongezekeo la mahitaji ya kukaa karibukaribu mchana na huenda wakataka kulala nawe usiku ili wajihisi salama.

Fahamu mihemuko, mawazo na matatizo ya mtoto wako. Mpe mtoto wako muda na kuwa karibukaribu anavyohitaji ili kuchochea kuwepo kwa hali njema na usalama. Kumbuka kuwa mihemuko yako binafsi inaweza kupitishwa kwa urahisi hadi kwa mtoto wako, hivyo jaribu kutulia ikiwa unahisi wasiwasi.

Wasiliana na huduma za matibabu ikiwa una swali lolote au chochote ambacho huna uhakika wacho. Tupo hapa ili kukusaidia.