Kutokula wala kunywa chochote

Tafadhali fuata maagizo yoyote ya kutokula wala kunywa kwa mdomo uliyopewa.

Hii ni kutokana na hatari ya chakula au vioevu kurudi kutoka tumboni hali inayoweza kusababisha matatizo mabaya sana kwenye njia za hewa na mapafu. Kwa hivyo kuwa mkweli wakati wote unaposema muda ambao mtoto wako amechukua tangu alipokula au kunywa, hata ikiwa hii itamaanisha huenda ukasubiri au kuwa upasuaji unahitaji kufanywa baadaye.

Vioevu vinahitaji muda mfupi zaidi wa kotokula wala kunywa chochote kuliko chakula kigumu. Hata hivyo, vinywaji tofauti vinahitaji nyakati tofauti za kutokula wala kunywa chochoote. Kwa mfano, sharubati na gururu zinahitaji muda mrefu kupita kuliko maji, vinywaji baridi na kahawa. Maziwa ya mama na maziwa ya fomula ni kati ya kioevu na chakula kigumu. Wasiliana na hospitali ikiwa hujaelewa chochote katika maagizo ya kutokula wala kunywa chochote uliyopewa.