Kutathmini maumivu kwa watoto

Tathmimi ya maumivu ya mara kwa mara hufanywa ili kuamua ukubwa wa maumivu, maumivu yalipo na athari ya kitulizo cha maumivu. Watoto wengi wanaweza kuwaambia wafanyakazi kuhusu maumivu yao wenyewe na wazazi wanaweza kusaidia pia mara nyingi.

Kutathmini maumivu kwa mtoto aliyezaliwa na mtoto mchanga linaweza kuwa jambo gumu. Katika hali hii ya watoto wadogo sana matokeo ya maumivu yanatumiwa kulingana na aina tofauti za tabia. Zana za kupima maumivu zinaweza kutumiwa kutegemea na umri na kiwango cha uelewa cha mtoto. Hapa, kipimo cha nyuso na kipimo cha nambari kutoka 1 hadi 10 hutumiwa sana.