Ikiwa mtoto wangu ana maumivu

Maumivu yanaweza kutofautiana: yanaweza kuwa mabaya anapojishughulisha na bora anapopumzika. Mtoto anaweza kuwa na maumivu anapopumzika, kulala au kucheza.

Fuata mapendekezo ya kitulizo cha maumivu uliyopewa hospitalini. Mchanganyiko wa dawa zinazofanya kazi kwa njia tofauti ndio bora. Tilia mkazo sheria haswa inapohusu aina ya dawa, dozi, na wakati wa dozi ili kuimarisha kiwango cha kitulizo cha maumivu na kuepuka “maumivu kupanda”.Hii inatumika hata ikiwa mtoto wako haonekani kuwa na maumivu kwa sasa.

Mwamshe mtoto ili umpe kitulizo cha maumivu wakati wa usiku, hata ingawa si vizuri kuusumbua usingizi wake. Watoto na vijana kwa kawaida hurudi kulala haraka. Hii huzuia ongezeko la maumivu yanayoweza kuusumbua usingizi na huenda vikawa vigumu kukabiliana siku inayofuata. Kitulizo cha maumivu cha mara kwa mara pia kinamaanisha kuwa viwango vidogo vya dawa vinahitaji kupewa kwa jumla, jambo linalopunguza athari zinazotokana na dawa.

Kujishughulisha ni njia ya asili ya kusaidia maumivu. Unaweza kushughulisha akili za mtoto wako kwa kumwomba kufikiria kitu cha kufurahisha, au kitu anachopenda kufanya. Mhimize acheze michezo, asome, achore, aimbe, apige gumzo mtandaoni au atazame video. Pia unaweza kusaidia kwa kubadilisha alivyolala kitandani, au kwa kuweka mto chini ya mkono au mguu au nyuma ya mgongo wake. Baada ya upasuaji wa koo, kunywa au kula kitu baridi au kunyonya barafu yote ni mambo yanayotuliza.

Kutembeatembea husaidia siha na mwili kuzalisha kitulizo chake cha maumivu. Fuata sheria ulizopewa kuhusu kutembeatemba na umwulize mfanyakazi sheria zinazotumika baada ya mtoto wako kufanyiwa upasuaji. Mchachawishe na umhimize mtoto wako kutembeatembea kwa njia tofauti kwa mujibu wa sheria. Katika visa vingi kuna mazoezi ya mwili ambayo mtoto anaweza kuruhusiwa kufanya licha ya vikwazo. Watoto na vijana wote hufurahia hewa safi, mazoezi ya mwili na kutembeatembea wakati mili na akili zao zinapaswa kurejea kutokana na kukaa hospitalini.

Wasiliana na huduma za matibabu ikiwa una swali lolote au kitu chochote ambacho huna uhakika kuhusu udhibiti wa maumivu ya mtoto wako. Tup hapa ili kukusaidia.