Haki ya watoto na vijana kupata taarifa na maandalizi

Watoto na vijana wanataka kujua kitakachowatendekea na wanataka kuhusishwa katika huduma ya utunzaji wao. Kwa utunzaji na matibabu, ni haki ya kisheria kuwa na taarifa na maandalizi kwa njia ambayo mtoto au kijana anaweza kuelewa na kutekeka kifikra.

Mapatano ya Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Watoto (1989) yanalenga kuhakikisha kuwa maslahi bora ya watoto na vijana yanapewa kipaumbele katika hali zote. Mapatano yanabainisha wazi kuwa watu wazima wanawajibika kuwahusisha watoto na vijana katika huduma ya afya na matibabu yao binafsi. Wana haki ya kuheshimiwa, kuruhusiwa kutoa maoni yao, kuhusishwa na kupewa taarifa.